Na Heri Shaaban
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewapongeza viongozi wa dini kwa kudumisha amani na kuleta maendeleo nchini.
Mpogolo amesema hayo, Dar es Salaam, katika maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 19 ya Kanisa la WRC Kivule, wilayani Ilala, ambapo alimwakilisha Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila katika maadhimisho hayo.
"Nitumie fursa hii kuwapongeza viongozi wa dini kwa mchango wenu mkubwa wa kudumisha amani pamoja na kuleta maendeleo ya jamii katika nchi yetu alisema" Mpogolo
Amesema licha ya changamoto mbalimbali viongozi wa dini wanaendelea kujitoa kwa kushirikiana na serikali katika shughuli mbalimbali kwa ajili ya mchango wao.
Pia Mpogolo ametumia fursa hiyo kuipongeza serikali ya Dk. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi za kuleta maendeleo katika nchi na fursa mbalimbali za kiuchumi na utoaji fedha nyingi katika mkoa huo ambapo mafanikio hayo yote yamepatikana kwa ya viongozi wa dini kudumisha amani
Amesema viongozi wa dini wamekuwa nguzo muhimu katika kuleta amani,utulivu,upendo na mshikamano miongoni mwa wananchi na kujenga jamii kupitia hofu ya Mungu hali inayochangia kwa kiasi kikubwa utekelezaji wa malengo ya serikali .
Wakati huo huo, Mpogolo amewataka waumini na wananchi kuendelea kumuombea Rais Dk. Samia na kudumisha amani nchi yetu ya Tanzania.



