Na MWANDISHI WETU
Diwani Kata ya Ilala Saady Khimji, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia Januari hadi Juni 2026.
Akiwasilisha taarifa hiyo, Khimji amesema Kata ya Ilala imefanya mambo makubwa na inakuwa kata ya kisasa kutokana na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kufanya kazi kubwa kwa kushirikiana na Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu.
Khimji ametaja baadhi ya mambo aliyotekeleza kipindi cha miezi sita yakiwemo, afya, mazingira, ujenzi wa Zahanati ya Bungoni, mapokezi ya vifaa mbalimbali ya vifaa vya Zahanati ya Kisasa Bungoni.
Pia uzoaji wa taka ngumu, majitaka na majisafi, masuala ya lishe, ulinzi na usalama, sekta ya elimu msingi na Sekondari, maendeleo ya jamii na miundombinu ya barabara.
Akizungumzia sekta ya afya amesema Zahanati ya Ilala Bungoni, ujenzi wa vyoo vya nje unaendelea ambapo kunajengwa matundu matatu ya vyoo na choo cha watu wa makundi maalum, ujenzi wa stoo,mnara wa tanki, na ujenzi wa fensi.
"Nawashukuru wajumbe wote wa kata hii walipiga kura kwa wingi na ushindi wa kishindo katika uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani ambapo ushindi mkubwa CCM umepatikana Ilala, kura za Rais Dk. Samia na Mbunge wetu Musa Zungu ambapo CCM imeibuka kidedea "amesema Khimji.
Kimji amezungumzia sekta ya elimu kuwa Ilala ina shule ya msingi saba na shule za Sekondari tano, kati ya hizo shule tatu za sekondari za msingi na serikali na tatu za binasfi.
Amesema Shule ya Msimbazi Mseto imefanikiwa kupata mradi wa madarasa matatu mradi umekamilika na Sehemu zingine wako katika hatua za mwisho gharama za mradi huo ni shilingi milioni 217, Shule ya Msingi Ilala shilingi milioni 30,000,000, ukarabati madarasa mawili na shule ya msingi Mkoani vyumba sita na Ofisi ya mwalimu mkuu gharama za mradi shilingi 90,000 ,0000/=
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Kata ya Ilala, Habib Nasser, amempongeza Khimji kwa kuwasilisha Ilani ya Chama.
Pia amempongeza na Rais Dk. Samia kwa kuwekeza niradi mikubwa ya maendeleo Ilala.
Aidha Nasser amewataka watendaji wa kata hiyo na watumishi wake kufanyakazi kwa weledi, kushirikiana na Chama na serikali katika na kutatua kero za wananchi.



