​Wasomi wa Chuo Kishiriki Mkwawa Wagundua Tiba na Marashi Kupitia Zao la Ulanzi


Washiriki wa  Maonesho ya Kimataifa ya 50 ya Biashara katika banda la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) wamesema mwaka huu, kupitia maonesho hayo wamekuwa na mapinduzi makubwa ya ubunifu kwenye sekta ya Elimu.

Akizungumza katika maonesho hayo, Mhadhiri Mwandamizi kutoka Idara ya kemia Chuo kishiriki cha Elimu Kwawa,  Dk. Lewis Mtashobya amesema kupitia maonesho hayo wamekuja na ubunifu wa hali ya juu kupitia zao la ulanzi.

Amesema kupitia Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa, wanao mradi wa kutengeneza Bayoritano inayotokana na  zao la Ulanzi.

Mtashobya amesema zao la ulanzi linatokana na utengenezwaji wa kinywaji cha pombe kutoka mikoa ya Kanda za juu Kusini, ikiwemo Mkoa wa  Iringa, Mbeya, Njombe, Songea na Songwe.

Amesema kwa kila mwaka kinywaji kicho kimekuwa kikishuka thamani kutokana na baadhi ya watu kukata miti ya mihanzi na kuharibu maziringa pia kupeleka kupoteza thamani ya zao hilo na wakulima kupata hasara ya kukosa wateja na hatimaye kuishia kukimwaga kinywaji hicho.

"Kinywaji cha ulanzi kinashuka thamani mwaka hadi mwaka, ambapo kwa mwezi Februari hadi Mach 2026, Lita moja ya kinywaji cha pombe ya Ulanzi inauzwa shilingi mia mbili.

Mtashobya amesema wao kama wasomi wameamua kufanya tafiti wa kuliongezea thamani zao la ulanzi na kisha kuja na mwarobaini  wa tiba kwa kuongezea bidhaa mbalimbali ikiwemo marashi ya kunukia (Pafyum) na dawa za hospitalini.