Na MWANDISHI WETU
Mamlaka ya rufani ya zabuni za Umma (PPAA) imewataka wananchi kutembelea banda hilo katika maonesho ya Saba Saba, wajifunze mambo mbalimbali yanayofanywa na taasisi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Sehemu ya Huduma za Sheria PPAA, Agnes Sai amesema huduma zinazotolewa na taasisi hiyo zinaleta tija ndani ya nchi na jamii kwa ujumla.
amesema PPAA kwa mwaka huu wa fedha uliyoishia 2025-2026 imepokea rufaa takribani 60 na kufanikiwa kutoa uwamuzi wa rufaa 58 huku rufaa mbili wanasubiri wasiwasirishe kwenye bajeti ya mwaka huu 2026-2027, zifanyiwe kazi.
Kwa upande wa utoaji elimu, Agnes amesema taasisi hiyo imeweza kutoa elimu kwa wadau wao wapatao elfu 2600, wazabuni wakiwemo elfu 1907 na watumishi wa Umma 705.
Ambapo ameeleza majukumu ya taarifa hizo zinapatikana kupitia website yao na kupelekea kujua taarifa zozote zinazotolewa na PPAA.
