AskofuMkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Cardinal Pengo, amefariki dunia tarehe 19 Februari 2026, saa 4:00 usiku.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Thaddeus Ruwaichi, imeeleza kuwa Kardinali Pengo amefariki akiwa anapatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
“Ninayo masikitiko makubwa kuwatangazieni kwamba leo tarehe 19/02/2026 saa 04:00, usıku mpendwa baba yetu Mwadhama Polyearp Cardinal Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jımbo Kuu la Dar es Salaam, ameitwa nyumbani kwa Baba wa Milele akiwa katıka Tasısı ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jijini Dar es Salaam.
Taarifa za mazishi zitawajia baada ya mipango kukamilika. Tumwombee apumzike kwa amani.
Raha ya milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele Umwangazie, Apumzike kwa Amani; Amina.”


Social Plugin