Na Sixmund Begashe, Same
Wananchi 1,690 wamelipwa kifuta jasho na kifuta machozi chenye Juma ya shilingi 410,905,000 kutokana na madhara yaliyosababishwa na Wanayamapori wakali na waharibifu kwa mwaka wa fedha 2024/2025 Wilayani Same na Mwanga Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji ameyasema hayo katika ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba katika mkutano wa hadhara uliofanyika Wilayani Same Mkoani Kilimanajaro na kuongeza kuwa , Serikali chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanya maboresho ya viwango vya vifuta machozi na vifuta jasho vinavyotolewa kwa wananchi wanaoathiriwa na Wanyamapori wakali na waharibifu sambamba na kuweka mfumo wa kielektroniki ili kuhakikisha waathirika wanapata kifuta jasho na kifuta machozi kwa wakati.
Dkt. Kijaji amewahakikishia wananchi hao, kuwa Wizara hiyo itaendelea kushirikiana nao kikamilifu katika kuhakikisha wanaendelea kunufaika na uhifadhi kama ilivyo dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwaongezea wananchi furaha na tabasamu kwa kuwainua kiuchumi.
Dkt. Kijaji, ameongeza kuwa, uwepo wa Hifadhi ya Taifa Mkomazi na Hifadhi ya Msitu wa Mazingira Asiliana Chome ni chachu ya maendeleo ya wananchi hususani wa maeneo ya same kwa kuwa unatengeneza ajira na kuchangia katika pato la Taifa linalopelekea maboresho kwenye sekta mbalimbali hususani afya, Elimu na miundombinu.




Social Plugin