Balozi Mulamula afanya mazungumzo na Neema Lugangira, Addis Ababa Ethiopia


Na MWANDISHI MAALUMU

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Afrika wa Masuala ya Wanawake, Amani na Usalama, Balozi Liberata Mulamula, amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Women Political Leaders (WPL), Neema Lugangira, kuhusu ushirikiano wa kikazi katika kuwaendeleza wanawake.


Akizungumza jijini Addis Ababa, Ethiopia, leo, Balozi Mulamula alisema amefurahi kukutana na kiongozi huyo ofisini kwake nakujadiliana naye masuala mbalimbali ya kuwaendeleza wanawake.


"Nimefurahi kukutana na Neema Lugangira ambaye kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Women Political Leaders (WPL), nimempongeza kwa nafasi hiyo na kumuahidi ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yake. Kiongozi huyu namfahamu nilikuwa naye bungeni Tanzania, ni mchapakazi na, mpenda maendeleo naamini atakuwa msaada mkubwa kwa wanawake," amesema.


Amesema katika mazungumzo yao, wamejadiliana kuimarisha ushirikiano wa wanawake katika siasa, hususan katika muunganiko wa amani, usalama na misaada ya kibinadamu; na wamekubaliana kushirikiana kupitia ofisi zao.


Kwa upande wake, Katibu wa WPL, Neema Lugangira, amempongeza Balozi Mulamula kwa kwa kuteuliwa kuwatumikia wanawake wa Afrika na utumishi uliotukuka anaoendelea nao huku akimuahidi ushirikiano katika utekelezaji majukumu yake.


Balozi Mulamula afanya mazungumzo na Neema Lugangira, Addis Ababa Ethiopia Balozi Mulamula afanya mazungumzo na Neema Lugangira, Addis Ababa Ethiopia Reviewed by Gude Media on 10:48:00 PM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.