Rais Dk. Samia afanya uteuzi wenyeviti wa bodi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa wenyeviti wa bodi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, walioteuliwa ni Anne Makinda, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Usimamizi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS).
Jaffer Machano ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC). Jaffer anachukua nafasi ya AllyAmani Karavina.
Dk. Albina Chuwa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kituo cha Taifa cha Ufuatiliaji wa Kaboni (NCMC) na Profesa Makenya Maboko, ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Tume yaVyuo Vikuu Tanzania (TCU).
Rais Dk. Samia afanya uteuzi wenyeviti wa bodi
Reviewed by Gude Media
on
6:20:00 AM
Rating:
Reviewed by Gude Media
on
6:20:00 AM
Rating:


No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.