Wakazi Ilala wahimizwa utunzaji mazingira kwa kupanda miti
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuendeleza uzalendo wa kweli kwa kutunza mazingira Kwa kupanda miti na kuitunza.
Mpogolo, ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, yaliyofanyika katika shule ya wasichana Jangwani.
Mpogolo amesema kuwa uzalendo wa kweli huanzia katika vitendo vinavyolinda rasilimali za Taifa, hususan mazingira.
"Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amekuwa mstari wa mbele katika utunzaji wa mazingira. Hivyo, tunapoadhimisha siku ya kuzaliwa kwake, tunapaswa kufata maono yake kwa kupanda miti, kwani unapopanda mti unatunza mazingira na unaweka msingi wa maisha bora kwa kizazi kijacho," amesisitiza Mkuu wa Wilaya.
Aidha, Mpogolo ametoa wito kwa wananchi wa Ilala kuhakikisha kila kaya inapanda miti isiyopungua mitatu, huku akiwataka wakuu wa shule na Taasisi mbalimbali kusimamia ipasavyo upandaji na utunzaji wa miti ili kuhakikisha inaleta tija iliyokusudiwa.
Awali Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, amesema kulingana na kaulimbiu 'Uzalendo ni kutunza mazingira, shiriki kupanda miti', Halmashauri imejipanga kupanda miti zaidi ya milioni moja katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo, sambamba na kuimarisha utunzaji wa mazingira na matumizi ya nishati safi.
Reviewed by Gude Media
on
8:22:00 AM
Rating:



No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.