Baraza la madiwani Kinondoni lapitisha bajeti ya Sh. bilioni 178.9 kwa mwaka wa fedha 2026/27


BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Mkoa wa Dar es Salaam, limepitisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya kawaida ya miradi ya maendeleo ya sh. bilioni 178.9 katika mwaka wa fedha 2026/27.

Akizungumza katika kikao cha baraza hilo, Dar es Salaam, Meya wa Halmashauri hiyo, Songoro Mnyonge, amesema katika kiasi hicho, sh. bilioni 86.03 ni ruzuku kutoka serikali kuu sawa na asilimia 48.

 Ameeleza sh. bilioni 92.9 ni fedha za makusanyo na ndani ya halmashauri hiyo sawa na asilimia 52.

“Kiasi cha sh. bilioni 46.04 sawa na asilimia 70 ya mapato ya ndani ambayo ni asilimia 34 ya bajeti yetu kina kwenda katika utekelezaji wa miradi,” ameeleza Meya Mnyonge.

 Amesema manispaa hiyo imejipanga kikamilifu kutekeleza miradi ya maendeleo hivyo kuwashukuru madiwani kwa kupitisha makadirio hayo ya bajeti. 


Baraza la madiwani Kinondoni lapitisha bajeti ya Sh. bilioni 178.9 kwa mwaka wa fedha 2026/27 Baraza la madiwani Kinondoni lapitisha bajeti ya Sh. bilioni 178.9 kwa mwaka wa fedha 2026/27 Reviewed by Gude Media on 8:20:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.