UNICEF yawataka walimu wa MEMKWA kuwajibika kulingana na mafunzo waliyopewa


Mratibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Elimu Msingi ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Jackson Kamana amewataka Walimu wa Mpango wa Elimu ya Msingi kwa watoto waliyoikosa (MEMKWA) kuwajibika kulingana na mafunzo waliopatiwa.


Kamana ametoa wito huo leo Jumamosi Januari 31, 2026 wakati akifunga mafunzo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid yaliyofanyika katika ukumbi wa Maxwel mjini Igunga.


Ameeleza kuwa Igunga kuna vituo vya MEMKWA 37 ambapo takwimu zinaonesha kunaongezeko la wanafunzi wanaojiunga na vituo hivyo.


Amewaambia walimu hao UNICEF imekwishawapatia takribani sh. Milioni tatu kwa lengo la kuendeleza kampeni kuhakikisha wanafunzi ambao hawako kwenye mfumo rasmi wanajiunga na masomo. 





UNICEF yawataka walimu wa MEMKWA kuwajibika kulingana na mafunzo waliyopewa UNICEF yawataka walimu wa MEMKWA kuwajibika kulingana na mafunzo waliyopewa Reviewed by Gude Media on 5:55:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.