Utitiri wa ving'ora barabarani, namba za magari serikali yatoa tamko
Ametoa rai hiyo wakati wa ziara katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ambapo alifika kwa mara ya kwanza baada ya kuteuliwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuongoza wizara hiyo ambapo aliambatana na Naibu Waziri,Ayoub Mohamed Mahmoud.
‘Gari la Zimamoto linawasha king’ora ili mlipishe liende likatoe huduma ya dharura ya ajali,madereva wengi hawazingatii wala kushtuka na vile ving’ora na kuona kama ni jambo la kawaida,sasa ukikwamisha chombo cha dharura hatua zitachukuliwa dhidi yako na ninawasihi wananchi kuzingatia ving’ora vya gari za wagonjwa,zimamoto,misafara ya viongozi.Na sasa serikali tuko katika hatua za mwisho ili kudhibiti ving’ora ambapo sasa imekua ni vurugu kila mtu anafunga na sasa tunaenda kuviondoa.’ Amesema Waziri Katambi
‘Nchi yetu inaongozwa kwa taratibu na sheria, Jeshi letu la Zimamoto linalaumiwa halifiki kwenye matukio kwa haraka lakini sio kweli,kumekuwepom na watu kutofuata kanuni za ujenzi mtu anajenga kwenye njia,wengine wanakwepa ukaguzi wa vifaa vya zimamoto kwa kukimbia gharama lakini gharama kubwa zaidi ni kupoteza maisha na mali hivyo ndio inatakiwa viwe vipaumbele vya kwanza katika ujenzi wowote ule.Sasa unakuta sehemu kuna janga lakini njia hazipitiki askari wetu watafikaje eneo la tukio", amesema.
Utitiri wa ving'ora barabarani, namba za magari serikali yatoa tamko
Reviewed by Gude Media
on
6:22:00 AM
Rating:
Reviewed by Gude Media
on
6:22:00 AM
Rating:





No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.