IGUNGA - TABORA
IKIWA zimesalia siku tano kumalizika mwaka wa Fedha 2025 hadi 2026 na kuanza mwaka 2026 mpaka 2027 Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Bi. Selwa Hamid ameendelea kuwashukuru na kuwapongeza Watumishi wote kwa kazi wanazoendelea kuzifanya kuwahudumia wananchi.
Selwa ametoa shukran hizo wakati wa mwendelezo wa ziara yake kutembelea Idara na Vitengo katika Halmashauri hiyo mjini Igunga.
Akizungumza na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, John Tesha, Selwa amesema ni lazima wajitahimini kwa kazi walizozifanya katika mwaka huu unaoisha na kuweka malengo mapya katika mwaka huo mpya wa fedha.
"Nimekuja kuwashukuru kwa kazi nzuri na kuwatia moyo tuendelee kufanya kazi vema," amesisitiza.
Kwa upande wa elimu mbali na kuwapongeza, Selwa amesema Halmashauri hiyo ni kubwa lakini viongozi hao wanafika katika shule zote na wanafanya vizuri, hivyo hana budi kuwashukuru kwa kazi wanazozifanya na kuendelea kuhimiza kudumisha ushirikiano.



