Kampuni ya Chilambo Yaibua Ubunifu wa Mikeka Inayotokana na Betri Chakavu


Yaiomba Serikali kuendeleza Ushirikiano

Na MWANDISHI WETU

Wadau mbalimbali wa masuala ya ubunifu wa teknolojia nchini, wameiomba Serikali iendelee kutoa ushirikiano wa kuwasaidia ili kuendana na mfumo wa  teknolojia na mazingira.

Meneja wa Kampuni ya Chilambo, anayehusika na masuala ya uchakataji,  Fretch Chilambo amesema hayo katika Maonesho ya Kimaaifa ya 50 ya Biashara, Dar es Salaam.

Amesema katika utafiti wao wametengeneza mkeka unaotokana na baadhi ya nyenzo (material) yanayotokana na betri na vyuma chakavu.

Aidha amesema kama Serikali ikitoa ushirikiano huo wao wataweza kubuni vitu mbalimbali vitakavyoweza kuongezea dhamani ya uchumi wa nchi.

Pia ameishukuru Baraza la Taifa la Hifadhi ya Mazingira (NEMC) kwa kuonyesha ushirikiano mkubwa katika maonesho hayo hasa ktuonyesha ubunifu wao kwa wananchi wanaofika kutembelea banda hilo.