Mwenyekiti wa Mtaa wa Karume, Bechina Awasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani


Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa wa Karume, Hajji Bechina, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kipindi cha Januari hadi Juni 2026.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama kwa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM tawi la Shauri Moyo, Bechina  amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake, Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Spika wa Bunge pamoja na Diwani wa Kata ya Ilala, Saady Kimji, kwa kupeleka fedha nyingi katika miundombinu ya barabara.

"Natumia fursa hii kumpongeza Rais wetu Dk. Samia barabara 26 zinazojengwa Ilala mtaa wetu wa Karume umenufaika pia haya ni maendeleo makubwa yamefanywa na Rais, Mbunge wetu Musa Zungu pamoja na Diwani Saady Kimji nawaomba wananchi wangu wa Karume tulinde hiii miradi ya maendeleo ambayo imetekelezwa na Serikali yetu" amesema Bechina.

Bechina amesema mikakati yao katika mtaa huo kwa kushirikiana na mkandarasi wa TARURA wataboresha miundombinu ya Barabara ya Mtaa wa Tabora.

Aidha amesema mikakati mingine kwa kushirikiana na Mkandarasi wa Kampuni ya Usafi SATEK na Wajumbe wa mashina watatoa elimu ya usafi na kuwataka Wananchi wachangie tozo ya Takataka kila mwezi ili mtaa huo uwe safi wa kuvutia. 

Amesema Kampuni ya Usafi ya SATEK ndio imebeba jukumu la usafi kata ya Ilala ikiwemo mtaa wa Karume ambapo inashirikiana vizuri na Serikali ya mtaa wake katika maswala ya usafi na mazingira pamoja na shughuli za kijamii.

"Serikali ya mtaa wangu katika kipindi cha January mpaka Juni 2026 imeweza kuwaunganisha wananchi katika vikundi vya uwezeshaji kiuchumi, waweze kupatiwa mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa na Serikali mikopo ya asilimia kumi ambayo aina riba.

Kwa upande mwingine aliwashukuru Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Tawi la Shauri Moyo kwa kushirikiana vizuri na Serikali ambapo chama na Serikali wanafanya kazi pamoja katika kutatua changamoto za wananchi.