Na MWANDISHI WETU
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limeongeza vituo tisa vya kutoa huduma za uokoaji Mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Zimamoto Duniani, Kamishina Msaidizi Mwandamizi kikosi hicho, Mkoa wa Ilala, Peter Mabusi, serikali imeboresha kikosi hicho kwa kuongeza vituo tisa vya kutoa huduma.
"Serikali ya Awamu ya Sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, imeboresha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa kujenga vituo tisa vya Zimamoto mkoani humo maeneo tofauti yakiwemo Faya Ilala, Legalo , Tazara, Kariakoo, Chanika, Mbweni, Standi ya basi Magufuli na Mwalimu Nyerere Posta", alisema Mabusi.
Pia Mabusi alisema wanamkakati wa kuongeza vituo vinne vya Zimamoto na Uokoaji katika maeneo ya Masaki , Kinyerezi, Kigamboni na Kivule.
Aidha Peter Mabusi alisema dhumuni la siku hiyo ya kilele cha siku ya Zimamoto Duniani ni kuwakumbuka Askari wa jeshi hilo waliopoteza maisha wakati wakitimiza majukumu yao nchini Australia, ambapo maadhimisho haya yanaanzia April 28 mpaka Mei 04 kila mwaka Duniani ndio kilele chake.
Alisema kauli mbiu ya siku ya Zimamoto Duniani "tuchukue tahadhari leo mwisho wa siku waweze kuokoa mali zao .
Akizungumzia changamoto ya miundombinu ya barabara katika mkoa huo zinapelekea jeshi la uokoaji kushindwa kufika kwa wakati kutoka na ujenzi holela wa majengo .
Aliwataka wananchi kutoa taarifa za ajali ya moto kwa kupiga simu namba 114 kuelezea eneo la ajali, huduma hiyo bure Jeshi la Uokoaji Zimamoto litafika kwa wakati na kuchukua hatua za uzimaji.


