Yanga yamfuta kazi Kocha Mkuu Pedro


Uongozi wa Klabu ya Young Africans Sports Club umemfuta kazi Kocha Mkuu wa kikosi cha kwanza Pedro Gonçalves.

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa klabu hiyo, imeeleza kuwa uongozi unamshukuru kocha Pedro Gonçalves kwa mchango wake alioutoa ndani ya klabu na unamtakia kila la kheri katika majukumu yake yajayo.

Katika kipindi hiki kikosi kitakuwa chini ya Kocha Abdihamid Moalin na Kocha Patrick Mabedi hadi mwisho wa msimu.