Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaamu, inachunguza kifo cha Mmiliki wa Kiwanda cha Xil Li, Bhaozang Li.
Taarifa kwa Umma iliyotolewa na Kamanda wa Polisi wa kanda hiyo, Jumanne Mrilo, imeeleza kuwa Mei 16, mwaka huu saa 08. 00 usiku Mabibo, mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Bhaozang Ge, miaka 50, raia wa China, mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa kitwacho XIL LI, alishambuliwa na walinzi binafsi wa kiwanda chake na kupelekea kifo
Upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili watuhumiwa wachukuliwe hatua zaidi kali za kisheria.
