BAKWATA Imetangaza Sikukuu ya Eid El Adh haa Mei 27


NA MWANDISHI WETU

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), imetangaza sikukuu ya Eid Ek Adh haa mwaka huu kwa mujibu wa kalenda ya Kislaamu itakuwa Mei 27 mwaka huu.

Akizungumza na Waandishi wa habari, Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania BAKWATA, Al haji Nuhu Mruma, amesema sikukuu  mwaka huu itasaliwa Kitaifa Mkoa Dar es Salaam, Mei 27 Siku ya Jumatano katika Msikiti wa Mfalume Mohamed 1V Makao Makuu ya BAKWATA wilayani Kinondoni.

Mruma amesema swala ya Eid  itasaliwa saa 1.30 asubuhi na kufuatiwa na Baraza la Eid.

Aidha amesema kwa niaba ya Mufti wa Tanzania Sheikh Dkt.Abubakari Zuberi,  aliwatakia Waislamu wote Tanzania maandalizi mema ya siku ya Eid.