Mwenyekiti wa CCM Ilala Sidde Atoa Agizo Chanika


Na MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala, Said Sidde, amewaagiz aviongozi wa Chama Kata ya Chanika wilayani humo kusimamia vikao na wanachama walipe ada kwa wakati. 

Sidde alitoa agizo hilo, Mei 10, Chanika jijini Dar es Salaam, katika kikao cha chama kuimarisha uhai wa Chama na kuwapongeza wanaccm wa kata hiyo kwa kushinda uchaguzi mkuu kwa kishindo.

"Nawapongeza wanachama wa CCM Kata ya Chanika kwa ushindi mkubwa, Chama kimeibuka kidedea pia natoa agizo kwa viongozi wa Chama kufanya vikao, wanachama kulipa ada, kubuni miradi Rasilimali fedha kwa ajili ya kukuza chama, msimamie utekelezaji wa Ilani viongozi wa chama na Jumuiya zake ", amesema Sidde  

Pia Sidde amewataka kuongeza wanachama kujenga mshikamano na umoja ikiwemo kuimalisha Junuiya za Wazazi, vijana na Jumuiya ya wanawake (UWT). 

 Aidha amewataka viongozi wa CCM, kutembea kifua mbele katika kuyatangaza mazuri yote yaliofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, ikiwemo utekelezaji wa Ilani.

Sidde ametumia fursa hiyo viongozi hao wa Chama kwa kushirikiana na Serikali pamoja katika utekelezaji wa Ilani.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti CCM Kata ya chanika, Yahaya matumbo, amewataka viongozi wa mashina kufanya kazi za Chama na kuitisha vikao na kutatua changamoto za Mashina.

Matumbo amesema dhumuni la mkutano huo kuimarisha uhai wa Chama na jumuya zake ambapo amesema CCM Chanika ina mshikamano mkubwa na Serikali wanafanya kazi vizuri kwa umoja na mshikamano.

Pia Matumbo amempongeza Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo kukuza uchumi kwa kuongeza fursa mbalimbali.

Naye, Fatuma Lomo Mjumbe wa Halmashauri Kuu Wilaya ya Ilala,  amewataka Chanika kufanya vikao vya Chama kwa wakati, pia kuchapa kazi za chama kwa ajili ya kutafuta dola.