Na MWANDISHI WETU
Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imewakamata watu 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao, ikiwemo kutoa vitisho na lugha za matusi mazito kwa watu mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaa, Jumanne Muliro, watu hao wamekamatwa maeneo ya Ubungo.
Muliro amesema kundi hilo baadhi yao wamebainika ni wafanyakazi wa Kampuni ya INNOVIX CALL CO LTD na OTAIGO FINANCIAL SERVICES COMPANY LIMITED inayojishughulishana ukopeshaji wa pesa kwa njia ya mtandao.
Amewataja watuhumiwa hao ni Renatus Mujwahuzi, Odilia Oswin, Theresia Brastius na wenzao 34.
Aidha Muliro amesema hatua zaidi zinachukuliwa kuwafikisha kwenye mamlaka zingine za kisheria.
