GNM Cargo watoa msaada wa Kompyuta Sekondari ya Benjamin Mkapa


Na MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Usafirishaji GNM CARGO watoa msaada wa kompyuta 10 na Projecta mbili, Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa, wilayani Ilala Mkoa wa Dar es Salaam.

Msaada huo ulitolewa na uongozi wa kampuni hiyo kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita ya Dk. Samia Suluhu Hassan katika kukuza sekta elimu.

Akikabidhi msaada huo Mkurugenzi wa GNM Cargo, Clinton Mathias Mbilinyi, amesema msaada huo alioukabidhi katika shule hiyo kuhamasisha wanafunzi waweze kusoma vizuri masomo ya mfumo wa TEHAMA wafaulu kwa wingi.

"Leo tumekabidhi projecta mbili na kompyuta kumi ni sehemu ya ahadi yetu ambayo tulitoa hivi karibuni ambapo pia tutajenga sehemu maalum ya kujisomea wanafunzi wa shule hii ya Serikali Benjamini Mkapa " alisema Mbilinyi. 

Kwa upande wake Mkuu wa shule hiyo, Joseph Deo, amepongeza kampuni hiyo kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika sekta ya elimu ya sekondari.

"Msaada huu mkubwa tuopokea kutoka Kampuni ya usafirishaji mizigo naomba wadau wengine kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwekeza katika sekta ya elimu", amesema.

Deo amesema shule ya sekondari Benjamini William Mkapa ni serikali inajivunia kitaaluma kwa ufaulu mzuri mwaka hadi mwaka na ina mahabara ya kisasa.

Naye Kiongozi wa taaluma shule hiyo, Abdul Amani, amesema yeye kama wa taaluma shuleni hapo kwa niaba ya wanafunzi wezake msaada huo wa kompyuta na projecta mbili utawasaidia Katika masomo mbalimbali na kuongeza ufaulu shuleni.