Naibu Meya Ilala ataika Halmashuri ya jiji itenge maeneo ya utalii


Na Heri Shaaban, Dar es Salaam

NAIBU MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, John Ryoba, ameitaka halmashauri hiyo kutenga maeneo muhimu kwa ajili ya Utalii na sehemu za kupumzikia wageni .

Ryoba amesema hayo wilayani Ilala, Dar es Salaam, katika mpango mkakati wa Serikali wa miaka mitano 2026 mpaka 2030 .

"Jiji la Dar es Salaam tunaomba itangaze maeneo yake ya Utalii na kuyaorodhesha ili jamii iweze kuyatambua na kuyatumia kwa ajili ya kukuza utalii wetu wa ndani kwa wageni na Watanzania kwa ujumla", amesema.

Ryoba, amesema Soko la Kimataifa la Kariakoo, Ilala na maeneo mengine waliopo jijini humo yatambulike na kutangazwa ili yaweze kutumika na kuiongezea mapato Halmashauri wananchi wayatumie kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo kupumzika na wageni kula chakula mikusanyiko siku za Sukukuu na kupata fursa za kukuza uchumi wa nchi yetu.

Ryoba ameshauri mpango wa miaka mitano Ilala iweke dira kwa kutumia umeme wa sola katika maeneo muhimu ya Serikali na ya kupumzikia umeme ukikatika solar ifanye kazi 

Pia ameshauri Serikali iweke mpango mkakati kwa vijana wanaomaliza Sekondari na vyuo kwa ajili ya mazingira ya ajira na fursa .

"Mpango huu wa Serikali wa miaka mitano pia naomba waweke Watumishi kwa ajili ya kusaidia jamii ndani ya kaya pia katikati ya jiji la Dar es Salaam wasijenge nyumba badala yake watafutwe wawekezaji yajengwe magorofa kwa ajili ya madhari ya jiji hili pamoja n kuweka mkakati wa ujenzi wa madarasa na mabweni kwa wanafunzi wanaomaliza elimu ya msingi na sekondari", amesema.