Mbeto awataka wana CCM kujivunia rasilimali watu wake
Na Mwandishi Wetu , Zanzibar
Chama Cha Mapinduzi kimesema CCM ni taasisi kubwa imara yenye wanachama wengi wenye uwezo na fani tofauti hivyo Mwenyekiti wake hapaangiwi yupi wakufanya kazi naye kwa wakati upi na lini.
Aidha,CCM kimesisitiza kuwa kutokana na taasisi hiyo kuwa kubwa na tegemeo kwa Taifa,itaendesha kazi zake bila kupangiwa au kwa shindikizo.
Hayo yametamkwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Itikadi,Uenezi na Mafunzo, Khamis Mbeto Khamis aliyesema CCM kina hazina kubwa isiofilisika ya Viongozi wa chama na Jumuiya zake.
Mbeto alisema kila Mwanachama wa CCM mwenye uwezo, upeo na maarifa ya utendaji kazi za kisiasa, hupata nafasi kwa muda na wakati wake.
Alisema ndani ya CCM na kwenye Serikali zinazoongozwa na chama hicho ,kuna kazi nyingi ambazo zinawahitaji wanachama wenye uzalendo, nidhamu, utii na uvumilivu.
"Mwenyekiti wetu hapangiwi yupi au nani afanye naye kazi lini au kwa wakati gani na yupi anaetosha. Kwetu CCM kila mmoja ana hadhi na kufaa "Alisema Mbeto.
Aliwataka wanachama wa CCM kuwa watulivu, wenye staha, subira na maadili bila pupa au kiherehere.
"Kuna kazi nyingi.Tuko watu wengi na wote tunafaa kukifanyia kazi chama chetu. Hayupo yeyote peke yake ambaye ni bora zaidi ya mwingine"Alieleza.
Mbeto alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa kufuatia video ya mwana CCM mmoja, kutaka Mbeto akafanye kazi Tanzania Bara.
"Wapo watu hawakutegemea kama ningekuwa Mwenezi wa CCM Zanzibar. Hata mimi sikukuwa na ndoto ya kushika nafasi hii. Wakati ndio ulioamua na wakati mwingine unaweza kuamua vinginevyo "Alisema Mwenezi huyo
Reviewed by Gude Media
on
12:01:00 PM
Rating:


No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.