Na WANDISHI WETU
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Temeke, Hamis Slim, amewakata viongozi wa mabaraza, kamati za utekelezaji za kata na matawi za jumuiya hiyo kuvunja makundi yaliyotokana na uchaguzi mkuu wa Oktoba 29 , 2029 na kufanyakazi kwa ushirikiano.
Ameyasema hayo Dar es Salaam, leo katika ziara ya Kamati ya Utekelezaji ya jumuiya hiyo Wilaya ya Temeke, katika Kata za Kiburugwa na Kibondemaji inayo lenga kuwashukuru wanachama wa jumuiya hiyo kwa ushindi mkubwa wa CCM na kuimarisha uhai wa jumuiya.
Slim, amesema uchaguzi umekwisha hivyo ni wakati muafaka wa kuvunja makundi, kusameheana, kupendana na kuhudumia jumuiya kwa ufanisi na weledi.
“Tunawapongeza Jumuiya ya Wazazi mmeafanya kazi nzuri katika uchaguzi mkuu na kuipatia ushindi wa kishindo CCM na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Sasa ni wakati wa kuleta maendeleo. Tuzike tofauti zetu zilizotokana na uchaguzi. Mwiba ulipoingia ndipo unapotokea,”amesema.



