Katambi akutana na Balozi wa Burundi nchini Tanzania
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Burundi nchini Tanzania, Balozi Leontine Nzeyimana, jijini Dodoma.
Katambi na mgeni wake wamezungumza masuala mbalimbali ikiwemo uwepo wa kambi za Wakimbizi hapa nchini, Udhibiti na utoaji elimu ili kuzuia uhalifu na Ustawi wa Jamii ya Wakimbizi wa Burundi waliopo hapa nchini.
Kikao hicho, pia kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa wizara hiyo, Ayoub Mohammed Mahmoud , Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Maduhu Kazi na Ofisa wa Wizara ya Mambo ya Nje, Evans Magoiga.
Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Makao Makuu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Mtumba jijini Dodoma.
Katambi akutana na Balozi wa Burundi nchini Tanzania
Reviewed by Gude Media
on
10:38:00 AM
Rating:
Reviewed by Gude Media
on
10:38:00 AM
Rating:





No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.