Vikundi 88 vimepatiwa mkopo wa bilioni 1. 2 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga


 IGUNGA - TABORA

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, John Tesha amesema serikali inaendelea  kuwatendea haki wananchi wake kwa sababu wanakikundi 408 kutoka kwenye vikundi 88 wamenufaishwa na sh. 1.2 bilioni.


Tasha ameyaeleza hayo wakati wa Hafla ya kukabidhi  hundi kwa vikundi vilivyokidhi vigezo kupata mkopo iliyofanyika katika ukumibi wa Halmashauri hiyo mjini Igunga.


Aidha, ameikumbusha jamii kuwa utoaji wa mikopo hiyo ni endelevu huku akiwasisitiza waliokopeshwa kutekeleza  miradi waliyoombea fedha na siyo vinginevyo.


"Hakika tunaendelea kuishukuru serikali ya Awamu ya Sita ambayo imeendelea kuajiri Maofisa Maendeleo ya Jamii ambao wanaendelea kutoa elimu kwa wanachi kuhusu  namna bora ya kupata mikopo hii ambayo mchakato wake unaanzia ngazi ya kata," amesema. 




Vikundi 88 vimepatiwa mkopo wa bilioni 1. 2 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Vikundi 88 vimepatiwa  mkopo wa bilioni 1. 2 Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Reviewed by Gude Media on 1:59:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.