Mbeto: Rais Dk. Samia amethibitisha uzalendo na uungwana alionao


Na Mwandishi  Wetu, Zanzibar 


Chama Cha Mapinduzi  kimesema hotuba  iliotolewa na Rais Dk Samia  Suluhu  Hassan  alipozungumza na Wazee wa Mkoa wa Dar  Es Salaam ,ameonyesha kina cha uelewa alionao, ukomavu  na uungwana wake kisiasa  .


Pia CCM kimeitaja hotuba  hiyo  imeshiba  uzalendo, historia na yenye  kuhimiza  haja  na nia ya  kuendeleza dhima ya  Umoja  wa Kitaifa .


Hayo yameelezwa na Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC Zanzibar  , Idara ya Itikadi   , Uenezi  na  Mafunzo, Khamisi  Mbeto Khamis  aliyeitaja hotuba  hiyo kuwa  imeweka  msimamo thabit wa  kulinda uhuru , Amani na utulivu.


Mbeto  alisema matamshi ya Rais  Dk Samia yamewataka viongozi  wa madhehebu  za Dini  kuacha kuingilia medani za Siasa  na kuipangia hatma  Serikali na kusisitiza kuwa  Tanzania haina  Dini bali wananachi wake ndio wenye  imani za Dini. 


Alisema hotuba hiyo ya Rais  licha ya kuwa ni ya  kizalendo ,imetoboa ukweli  unaowataka Watanzania wote kujiona  wako sawa mbele ya katiba na kuwataka waendelee  kushi bila chuki,hasama au ubaguzi .


"Rais Dk  Samia ametoa hotuba  inayohimiza shime ya  Umoja, Uzalendo na upendo kwa Taifa.  Amewataka viongozi  wa Dini waendelee  kuwalea kiroho waumini wao bila ishara ya kulivuruga Taifa " Alisema Mbeto 


Aidha,  Mwenezi  huyo alisema Rais alihimiza ipo haja ýa watu kutotofautiana  kwani njia pekee kupata  muafaka ni  kukaa  pamoja mezani, kujadiliana , kuzumgumza hatimae kupata  suluhisho  .


'Kila jambo gumu  katika chini ya jua yoyote  linazungumzika mezani . Rais Dk Samia  hilo  ameliweka   bayana na kusisitiza hata marekebisho ya  katiba mpya ýanawezekana na kufikia tamati   "Alieleza 


Pia Katibu  huyo Mwenezi  aliitaja nia ya Serikali  ya CCM si kupendelea upande wowote   wa madhehebu  za  dini  au vyama vya  kisiasa  ,badala yake aliwataka watanzania wote  kuheshimu sheria  za nchi  .


Mbeto  alisema  ana  hakika hotuba  ya Rais Samia imefungua ukurasa mpya ambao utawaweka  watanzamia wote mahali pamoja kama ilivyo utamaduni , mila na desturi  ya Watanzania .


'Rais  Dk Samia ameonyesha ushupavu na ujasiri  akiwa ndiye mkuu  wa Nchi. Pia ametumia muda wake kuyaeleza mataifa rafiki mipaka  yao wakiwa  washika dau wa maendeleo bila kuingilia  uhuru  wa Taifa letu, alisema Mbeto

Mbeto: Rais Dk. Samia amethibitisha uzalendo na uungwana alionao Mbeto: Rais Dk. Samia amethibitisha  uzalendo na uungwana alionao Reviewed by Gude Media on 6:36:00 PM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.