Mbeto awaita Diaspora kuwekeza Tanzania


Na Mwandishi  wetu,zanzibar

Chama Cha Mapinduzi  kimewashauri Watanzania wanaoishi Marekani katika Nchi  za  Falme za Kiarabu na Ulaya kufuata taratibu za kisheria  ili kuwekeza  miradi ya kiuchumi na Biashara Zanzibar


CCM kimeeleza tayari  Serikali zake zimeandaa mazingira wezeshi yanayotoa nafasi kwa  Watanzania na wageni  wenye  mitaji ya kuwekeza katika visiwa vya  Pemba na Unguja. 


Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  Zanzibar,  Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo  ,Khamis Mbeto  Khamis ameeleza  hayo alipotembelewa na  raia toka Canada na Marekani wenye asili ya Afrika. 


Mbeto akizungumza na  wageni hao ofisini kwake ,  alitoa wito kwa Watanzania walioko nje na ambao  wameshapata  uraia wa nchi nyingine,wajitahidi kuwekeza  miradi katika  Nchi zao za  Asili.


Alisema  kwa Watanzania  waliopata uraia wa Mataifa mengine ,wenye  mitaji na mipango  ya  kufanya  biashara , wasione woga badala yake  ,waje  kuja kuwekeza  Zanzibar  ambako  kuna   miundombinu ya uhakika. 


"Watanzania  na Waafrika waliopata Uraia  Canada, Marekani,Falme za Kiarabu au   Ulaya wawekeze  Zanzibar .Waje Tanzania zipo  fursa nyingi .Kuna  umeme ,majisafi,   barabara, Usafiri  wa Anga  na Majini kwa  saa 24  " Alisema Mbeto.


Katibu  huyo Mwenezi  alieleza  baada ya Waafrika wengi kuishi ughaibuni ,bila shaka sasa wamepata elimu ya kutosha, uzoefu na mbinu aidha  za  bisahara au  za kuanzisha kampuni kubwa . 


"Kuna Waafrika wanaoishi ugenini kwa miaka mingi wakifanya kazi zilizowapatia fedha na Mitaji. Njia pekee waje kuwekeza    Tanzania  ambako kuna    Amani na utulivu "Alisisitiza 


Hata hivyo  raia hao wa kigeni  wenye  asili ya  Afrika , wamemhakikishia Katibu  Mwenezi  huyo na  kuahidi kufikisha ujumbe kwa  wenzao na kuwataka  wachangamkie fursa hizo .

Mbeto awaita Diaspora kuwekeza Tanzania Mbeto awaita Diaspora kuwekeza Tanzania Reviewed by Gude Media on 10:27:00 PM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.