Mwenyekiti Halmashauri Wilaya ya Igunga, Hemed ahidi kuongoza kwa kasi kukuza uchumi na huduma za kijamii
IGUNGA - TABORA
MWENYEKITI Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Shabani Hemed ameahidi kuiongoza Halmashauri hiyo kwa kasi itakayoiwezesha kukua katika nyanja ya uchumi, afya na huduma nyingine za jamii.
Hemed ameyasema hayo wakati wa Mkutano wa kwanza wa Baraza la Madiwani uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri hiyo mjini Igunga.
Akizungumza katika baraza hilo, Mbunge wa Jimbo la Manonga wilayani humo, Abubakar Alli amewataka Madiwani hao kutofanya kazi kwa mazoea badala yake wafanye kazi kwa kasi na kujituma kwa sababu wananchi wanataka matokeo ya suluhisho la matatizo yao na sio sababu.
Naye Mbunge wa Jimbo la Igunga, Charles Kabeho ameeleza kuwa ataendelea kutoa ushirikiano kwa lengo la kuhakikisha wanafanya kazi ambazo Rais Dk. Samia Suluhu Hassan amezikusudia kuzifanya katika wilaya hiyo.
Reviewed by Gude Media
on
December 05, 2025
Rating:



