SMZ hata ikijenga barabara za dhahabu wapinzani watapinga-Mbeto


Chama Cha Mapinduzi Zanzibara kimesema  upinzani wa   Zanzibar  unachojua ni  kupinga   maendeleo kwasababu tu yemeletwa  na   SMZ hivyo hata kama zitajengwa barabara za dhahabu upinzani utapinga.


Pia CCM kimekumbusha  hata Nabii  Yusuf  alipingwa na makuhani  wa  Misri , aliposhika  madaraka akiwa Mtendaji Mkuu  wa dola  ya  kifalme huko Misri.


Hayo yameelezwa na Katibu wa Kamati  Maalum  ya NEC ya CCM  Zanzibar , Khamis  Mbeto Khamis   aliyesema mantiki  ya kuwepo  upinzani  si kupinga na kubeza hata kwa mambo ya msingi. 


Mbeto  alisema anashangaa kuuona upinzani   hususan ACT Wazalendo , bila aibu  viongozi wake wamekuwa wakiipinga juhudi za  maendeleo  ya kisekta  yanayoonekana.


Alisema   SMZ  chini  ya CCM, hata  ikijenga Barabara za dhababu   , Majengo  ya shule   kwa kutumia  matofali ya  Almasi na lulu ,    ACT  kitabeza na kuita  huo ni  mkaa wa kuni za mikarafuu.


Mbeto alikitaja  kitendo cha upinzani  kupinga kimaendeleo  ,haukuanzishwa na    ACT  , kwani  wapinzani  wa ASP  chini ya Hayati Rais Mzee   Abeid  Amani Karume pia  walimpinga  alipoleta maendeleo.


"Maendeleo  hayakuwepo  Zanzibar enzi za ukoloni .Bila aibu  vibaraka na wapinga  maendeleo  dhidi ya  serikali  ya  ASP hawakuacha kubeza  .Wapinzani  wa ASP  walidai SMZ  haijafaanya lolote "Alisema Mbeto.


Pia Katibu huyo Mwenezi  alisema   hata  Nabii Yusuf  alipingwa na wapinzani  wake   asifanikishe sekta ya  Kilimo cha   Umwagiliaji na kujenga maghala   hivyo  ACT  kinapopinga  maendeleo ni  asili ile ile ya upinzani.


'Makuhani  wa Misri  walimbagua Nabii Yusuf  wakidai hana asili ya Misri .Wakamwita mshamba toka kijijini  Canaan huko  Palestina. Akafayiwa vituko  akwane kuleta maendeleo. Alisimama imara akabadili  Misri  kwa muda mfupi  " Alieleza 


Katibu  Mwenezi   huyo alisema kwa bahati nzuri  , wananchi wa Zanzibar  wameshapevuka kifikra na kupata mwamko  hivyo  wanajua kutofautisha ukweli  na  porojo za wanasiasa uchwara 



"Wananchi wameshuhudia  shule za ghorofa  zikijengwa , barabara, masoko, Viwanja  vya Ndege, Bandari na Madaraja yakijengwa. Wanajua   kutofautisha kati  ya  Maendeleo  na WaanaSiasa  wapiga maneno  majukwani" Alieleza  . 


 Mbeto  alisema  hata  Mzee  Karume  alipotekeleza  malengo ya   ASP na ya kimajumui hatimae    Tanganyika na Zanzibar zikaungana  ,  alichekwa na wapinzani  wake . 


Katibu  huyo Mwenezi  alisema tabia ya  kupinga kila kitu   imekuwa   mila , desturi  na utamaduni kwa  upinzani wa  Zanzibar  lakini kwa  Maendeleo  yaliofanyika , kila mwananchi sasa amejua ukweli .