Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja yajivunia mafanikio taaluma


Na MWANDISHI WETU

UONGOZI wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja, umesema utaendelea kusimamia kikamilifu suala la nidhamu na kukuza taaluma itakayoifanya shule hiyo kuendelea kutoa wahitimu bora.


Aidha ungozi huo umesema unajivunia mafanikio makubwa  yaliyopatikana baada ya shule hiyo kuingia katika 10 bora  mkoani Dar es Salaam katika mtihani wa moko  wa kidato cha nne mwaka huu.


Hayo yameelezwa na Mkuu wa  shule hiyo Joram  Nkya katika mahafali ya 16 ya  wanafunzi wa kidato cha nne, jijini Dar es Salaam.


Nkya, amesema shule itaendelea kusimamia kikamilifu suala la nidhamu kwa wanafunzi ili kukuza taalumas na ufaulu.


“Shule  ya Sekondari Mnazi Mmoja ilianzishwa mwaka 2007.Imeendelea kufanya vizuri kitaaluma na kwa mara ya kwanza imeingia katika 10 bora  za matokeo ya  moko ya  kidato cha nne mwaka huu,”ameeleza  Nkya.


Amesema  wanafunzi wanao hitimu kidato cha nne mwaka huu ndiyo walioiletea sifa kubwa kitaaluma shule hiyo.


“Hawa ndiyo  kwa mara ya kwanzao walianza kuleta ufaulu   mzuri wakiwa kidato cha pili,”amebainisha.


Amesema wahnafunzi hao wanatarajiwa kuhitimu kidato cha nne  wameifanya shule hiyo kuingia katika shule 10 bora  katika Mkoa wa Dar es Salaam.


“Kwa mwaka huu Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja imeingia katika  10 bora  ikiwa kundi moja na shule za sekondari za Kibasila, Dar es Salaam, Jangwani, Pugu, Chang’ombe, Azania,  Benjamin Mkapa,   Zanaki na Jamhuri,”amesema Nkya.


Amesema hatua hiyo inafanya  shule kuongeza jitihada, ikiwa ni pamoja na kusimamia ubora wa taaluma na nidhamu.Katika suala la nidhamu  wazazi tunaomba mtatusamehe kwa sababu titakuwa wakali,”alieleza Mkya.


Nidhamu ya shule imeimarika sana. Tunaomba wazazi mtuwie radhi kwa sababu kuna wakati tuna kuwa wakali

Amegiza wahitimu wote  walioshona nguo zinazoacha waza magoti  kufunga kanga, mzazi kuagiza kuripoti  kwani siyo ustaarabu.


Alieleza shule bila  nidhamu hakuna taaluma hivyo msingi mkubwa wa shule hiyo ni nidhamu ya wanafunzi.


 Aliishukuru serikali  kujenga jengo la ghorofa la madarasa 20 na vyoo 43 ambalo  ujenzi wako uko katika hatua za mwisho kukamilika.


Aliomba wadau kusaidia shule hiyo mashine ya photo kopi na  kompyuta kwaajili ya kuandalia mithani mingi kwa wakati mmoja.

 

Awali  mgei rasmi katika mahafali hayo, Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Silent Ocean,  Elliot  Mujumba,  ameipongeza shule hiyo kwa kuimarisha taaluma na nidhamu.


“Sisi tunawataza wahitimu kama ni rasilimali ya kesho na wadau wakubwa wa biashara. Endeleeni kusimamia nidhamu  kwani mahara popote kukiwa na upungufu wa nadhamu huwezi kufanikiwa,”amesema Mujumba.


Amesisitiza wazazi  kuto kulifumbia macho  suala la malenzi na nidhamu kwa watoto.


“Wazazi  tukilea watoto katika njia inayo wapasa itasaidia. Pia tusimamie vipawa vyao.Kukuza kitu ambacho mtoto anacho ndani. Kukuza kipawa  ambacho mtoto amezaliwa nacho,”amesema.


Jumla ya wanafunzi 365 wanatarajiwa kuhitimu kidato cha nne katika shule hiyo, ambapo katika mahafali hiyo walitunukiwa vyeti.






Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja yajivunia mafanikio taaluma Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja yajivunia mafanikio taaluma Reviewed by Gude Media on 4:47:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.