Wanaushirika washauriwa kutumia hisa kwa uwekezaji

Ofisa Ushirika Mwandamizi Ndimolwo Laizer kutoka Tume ya Maendeleo ya Ushirika akitoa mada wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo wanaushirika wa mazao ya bustani Tunduma Hortculture Marketing Corperative  Society (TUHOMCOS), mkoani Songwe.

Na MWANDISHI WETU

Vyama vya Ushirika vimeshauriwa kutumia hisa za Chama cha Ushirika katika kuongeza thamani ya Ushirika hasa kwa kupitia Uwekezaji unaoongeza mapato na tija kwa Wanaushirika na kukuza Vyama.

Amesema hayo Afisa Ushirika Mwandamizi wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Ndimolwo Laizer akitoa mafunzo ya kuwajengea uwezo Wakulima wa mazao ya bustani wa Halmashauri  ya Mji Tunduma Mkoani Songwe Juni 9, 2025.

Amesema hisa Wanaushirika ni vyema zitumike kwa kuwekezwa kwa ridhaa ya Wanachama kupitia Mikutano mikuu  kuongeza mnyororo wa thamani ya uzalishaji kama vile kununua mashine za kuongeza thamani ili kuongeza mapato zaidi ya Chama kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo ya Ushirika.

Afisa Ushirika Bi. Flora Daud nae akitoa mada katika mafunzo hayo ameshauri Vyama vya Ushirika kuzingatia misingi ya ushirika, mgawanyo wa uongozi katika vyama vya Usirika, Ushirika kujiendesha kibiashara na kutumia njia  za kidijitali kujitangaza ili kuongeza wigo wa masoko ya  mazao ndani na nje ya nchi.

Mada nyingine zilizofundishwa katika mafunzo hayo ni pamoja na dhana ya TANSHEP ambayo humtaka mkulima kuanzia sokoni na kumalizia shambani kwa  kipato zaidi, Kanuni za kilimo bora cha mazao ya Bustani pamoja na Sera za Serikali juu ya Kilimo cha mazao ya Bustani.

Mazao ya bustani yanayozalishwa na Vyama vya Ushirika ni pamoja na viungo, mbogamboga, maua, matunda katika maeneo mbalimbali.


Wanaushirika washauriwa kutumia hisa kwa uwekezaji Wanaushirika washauriwa kutumia hisa kwa uwekezaji Reviewed by Gude Media on 9:15:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.