Mbeto: Maelekezo ya Mwenyekiti CCM ni maagizo ya utekelezaji kwa Chama

Na Mwandishi  Wetu, Dodoma

Chama Cha Mapinduzi kimesema kitahakikisha kinayafanyia kazi maelekezo yote yalioelekezwa na Mwenyekiti  wa CCM  Rais Samia Suluhu  Hassan katika  kupitisha  wagombea  udiwani, Uwakilishi na Ubunge.

Pia Chama kimesema huu ni wakati  sahihi wa kuwang'amua mapema  ni wagombea gani waaminifu na Wazalendo  kwa  chama na Nchi.

Katibu  wa Kamati  Maalum  ya NEC  zanzibar,  Idara  ya Itikadi, Uenezi  na Mafunzo  ,Khamis Mbeto Khamisi amesema maelekezo  yakiotolewa na Mwenyekiti  katika mkutano mkuu wa Taifa ni maagizo ya utekelezaji toka   matawi hadi Taifa.

Mbeto amesema CCM kina uzoefu wa kutosha  kutokana na tabia  ya kukatwa kwa  majina ya wanachama wenye utiifu na nidhamu kuachwa na  kupendekezwa wagombea wasiokubalika katika jamii.

Amesema ni lazima sifa za kila mgombea zitokane na  juhudi binafsi kwa chama ,uzalendo wake , historia na upendo alionao kwa nchi na chama kama vigezo na vipaumbele muhimu.

"Kwa ngazi zote toka matawi hadi Taifa tutayafanyia kazi maelekezo ya Mwenyekiti  wa CCM  Rais samia .Tutakuwa makini kupitisha  wagombea udiwani, uwakilishi na ubunge", amesema Mbeto.

Aidha, amesema lazima tukaangalie mwenendo wa kila mwanachama  kabla ya uteuzi na kujua kama mgombea huyo ana nidhamu, mtii wa siasa,  sera na itikadi ya chama anayeishi kimaadili na mwaminifu.

"Tunampongeza sana Mwenyekiti wa chama  Dk Samia kwa maelekezo  yake kwetu. Tunakwenda kuyasismamia yote na kutenda haki bila kufanya kinyume chake", amesema.

Pia Katibu  huyo Mwenezi  alisema kuteua au kupitisha wanachama mamluki , wasio na uzalendo  kwa nchi na si wenye imani na sera zetu ,wamekuwa wakitupa lawama na majuto.

"Wakati wa TANU tulipoteza jimbo la mbulu .Alipitishwa Chifu Amri Dodo akaachwa Padri Herman Serwat aliyeongoza kura za maoni . Karatu akaachwa Dk  Wilbroad Slaa akateuliwa Patric Qorro tukapoteza "Alieleza

Mbeto alisema hata Iringa Mjini Chama kilikipitisha jina la monica Mbega  akaachwa  Fredrik Mawakalebela  aliyeongooza kura  za maoni jimbo pia  litatuondoka .

"Mwenyekiti    ametukumbusha kwa nia njema  tutende  haki kwenye  vikao vyyote vya maamuzi . Upendeleo, ubinafsi na rushwa uwe mwiko wa milele  "Alisisitiza katibu  huyo Mwenezi

Mbeto: Maelekezo ya Mwenyekiti CCM ni maagizo ya utekelezaji kwa Chama Mbeto: Maelekezo ya Mwenyekiti  CCM  ni maagizo ya utekelezaji  kwa Chama Reviewed by Gude Media on 8:47:00 PM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.