Na MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ilala, Saidi Sidde, amepiga marufuku wanachama wa chama hicho walioanza kufanya kampeni za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Chama kabla ya wakati na kuwataka kusitisha haraka.
Sidde ametoa kauli hiyo katika Kata ya Msongola, Wilaya ya Ilala, wakati wa kupokea taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chma kwa kipindi cha kuanzia Januari hadi Juni 2026.
"CCM Wilaya ya Ilala inatoa onyo kwa wanachama wote
walioanza kufanya kampeni za kugombea uongozi ndani ya chama waache mara moja.
Hakuna anayejua kesho; hivyo wasubiri muda rasmi utakapofika na filimbi
itakapolia," amesema.
Sidde amewataka viongozi kusimamia maeneo yao kwa weledi na kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Amesema juhudi hizo zitasaidia kuongeza wanachama wapya, kuwasajili katika mfumo wa kielektroniki na kuhakikisha wanalipa ada zao kwa wakati.
Aidha Sidde amewataka wanachama wa CCM kuendelea
kudumisha umoja na mshikamano na kushirikiana kwa karibu katika
kuimarisha chama na Serikali.

.jpeg)
