Rais la Filamu Tanzania Rajabu Amiry Amesema Serikali Yatoa Leseni kwa Wasanii


Na MWANDISHI WETU

RAIS wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Rajabu Amiry, amesema ,Tasinia ya Filamu Tanzania imeingia katika hatua mpya baada ya kampuni ya (TAVIC) kukabidhiwa rasmi leseni ya CMO.

Akizungumza Dar es Salaam Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Amiry , amesema Tasinia ya Filamu Tanzania imekuwa ya kwanza kwa sekta ya kazi za sauti na picha kupata leseni hiyo inayoitwa Tanzania Audiovisual collection Ltd TAVIC kukusanya na kugawa mirabaha kwa wenye haki za kazi zenye vigezo vya sauti yenye picha na filamu (audiovisual ).

Aidha amesema kupatikana kwa leseni hiyo kunafuatia mchakato uliokuwa ukisimamiwa Serekali kupitia Ofisi ya hakimiliki Tanzania COSOTA.

"Katika kipindi cha mchakato TAVIC ilitakiwa kutimiza vigezo mbalimbali vilivyowekwa na Mamlaka hiyo ikiwemo kuweka dhamana ya shilingi milioni 250 kabla kupewa leseni rasmi ambapo vigezo hivyo vimetimizwa" amesema Amiry.

Amiry amesema hatua hiyo ya kupata leseni rasmi ya kazi inaifanya TAVIC kuwa taasisi ya kwanza nchini yenye jukumu maalum la kusimamia ukusanyaji na ugawaji wa mirabaha kw a wazalishaji wa maudhui ya sauti zenye picha jongefu na Filam. Aidha Amiry ametaka wadau wa kazi za audiovisual kujisajili hili kupata fursa izo",  amesema Amiry.