IGUNGA - TABORA
MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Selwa Hamid amewapongeza na kuwashukuru Watumishi wote kwa kazi wanazozifanya ambazo zimeleta mabadiliko chanya katika kutoa huduma kwa wananchi jambo ambalo limepeleka tabasamu kwa wananchi.
Selwa ametoa shukrani na pongezi hizo, wakati alipofanya ziara ya kushitukiza katika Ofisi za Vitengo na Idara zote za Halmashauri hiyo mjini hapa akitoa pongezi na hamasa kufunga mwaka wa fedha vema na kuuanza mwaka mpya wa fedha kwa ari na kasi ya kutenda vizuri.
Amesema yapo mabadiliko makubwa ya kiutendaji, hivyo amewaomba waendelee kuwa na utiyari wa kufanya majukumu ipasavyo ikiwemo kupata vya halali.
Aidha, ameendelea kuishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeendelea kuajiri Watumishi jambo ambalo limeendelea kuwa mnyororo wa kufikisha tabasamu kwa wananchi.
"Leo nimekua na ziara ya kuwatembelea, kuona hali inavyoendelea mnavyofanya kazi, hakika hongereni sana mmefikisha tabasamu kwa wananchi.’’ amepengeza.



