Utabiri wa Hali ya Hewa kwa Saa 24 Zijazo


Na Heri Shaaban

MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania TMA yatoa utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu leo Mei 26 /2025.

Kwa mujibu wa Taarifa ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inasema visiwa vya Unguja na Pemba,kasikazini mwa mkoa wa Morogoro ,Mkoa wa Kilimanjaro,Arusha na Manyara kutakuwa na Mawingu kiasi mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Aidha taarifa hiyo inasema katika mikoa ya Pwani ikijumuisha Visiwa vya Mafia ,Mikoa ya Tanga ,Dar es Salaam,Tanga na Lindi kutakuwa na hali ya mawingu kiasi mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

Taarifa hiyo ya TMA imeeleza kuwa mikoa ya Dodoma na Singida,Kusini mwa mikoa ya Morogoro,Kigoma ,Tabora na Katavi,Mikoa ya Kagera na Singida,Geita ,Mwanza na Simiyu,Mara,na mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya,Rukwa,Ruvuma na Songwe itakuwa na Hali ya Mawingu kiasi na vipindi vya jua.