Mashabiki wa Arsenal nchini Wajitokeza kwa Wingi Kipima Afya zao katika Fainali ya UEFA viwanja vya Posta, Kijitonyama


Na MWANDISHI WETU

TAASISI ya Saratani ya Ocean Road, imeungana na taasisi nyingine za afya katika banda la Wizara ya Afya katika viwanja vya Posta, Kijitonyama, kuangalia fainali ya UEFA Champion Leage.

Fainali hiyo ya UEFA inazikutanisha miamba ya soka barani Ulaya, Arsenal ya Ungereza na PSG ya nchini Ufaransa, ambapo mashabiki wengi wa Arsenali nchini Tanzania walijitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao.

Mashabiki hao wa Asernal walioudhuria katika viwanja hivyo walipata nafasi kupima afya zao katika banda la Taasisi ya Ocean Road pamoja na kupewa elimu kuhusu ugonjwa wa saratani.

Katika shangwe hizo mashabiki wengi walijitokeza kipima afya zao pamoja na kupata elimu kuhusu saratani mbalimbali kutoka Taasisi ya Saratani Ocean.

Wananchi wametakiwa kupima mara kwa mara kujua mwenendo wa afya zao, ikiwemo saratani mbalimbali, kwasababu saratani ukigundulika mapema ni rahusi kutibika.