NA MWANDISHI WETU
SHULE ya Sekondari Juhudi iliyopo Gongolamboto, wilayani Ilala, Mkoa Dar es Salaam, inajivunia kitaaluma kwa ufaulu mzuri matokeo ya kidato cha sita miaka mitatu mfurulizo.
Mkuu wa shule hiyo, Happynes Pallangyo, amesema hayo katika Mahafali ya 9 ya Kidato cha sita, ambapo wanafunzi 395 walitunukiwa vyeti.
Akizungumza katika mahafali hayo, Pallangyo, amesema matokeo ya NECTA kidato cha sita kuanzia mwaka 2023 ,2024 na 2025 wanafunzi wote wamefaulu kwa asilimia 100 kutokana na jitihada za walimu wake kwa kushirikiana na Wazazi na wanafunzi .
"Shule yangu ya Juhudi kitaaluma ipo vizuri matokeo ya NECTA miaka mitatu Mfurulizo matokeo wamefaulu mkubwa mwaka 2023 Daraja la kwanza 65 daraja la pili 118 daraja la tatu 32 ufaulu asilimia 100 ,mwaka 2024 daraja la kwanza 96 daraja la pili 148 daraja la tatu wanafunzi 25 ufaulu asilimia 100 mwaka 2025 matokeo ya Moco Mkoa daraja la kwanza 52 daraja la pili 185 daraja la tatu 100 ufaulu asilimia 100" alisema Pallangyo.
Mwalimu Pallangyo, alisema wanafunzi hao wa kidato cha sita 2026 kwenye mtihani wa Moco mkoa waliweza kupata daraja la kwanza wanafunzi 258 daraja la pili 107 daraja la tatu wanafunzi nane na daraja la nne mwanafunzi 1 daraja sifuri amna.
"Shule yetu ya Sekondari Juhudi takwimu za kitaaluma zimekuwa mwaka hadi mwaka kutokana na juhudi za walimu , uongozi wa shule,Wazazi na Wanafunzi pamoja na mitihani ya kujipima kila wakati na mitihani ya mwezi "alisema Pallangyo.
Aidha amesema jumla ya wanafunzi 395 wakiwemo wasichana 213 na wavulana 182 wamehitimu kidato cha sita mwaka huu 2026 ambapo kutokana na maandalizi mazuri wanafunzi wote wanaenda kupata Division one.
Amesema shule hiyo ya Serikali ilianzishwa mwaka 2002 wakati wa Manispaa ya Ilala kwa wakati huo ambapo iliwekwa jiwe la msingi na Mkuu wa mkoa Dar es Salaam Yusuph Rajabu Makamba kipindi hicho ikiwa na madarasa manne na wanafunzi 90.



