SACP Mkonda awatahadhalisha madereva nchini


Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Tanzania, SACP Wiliam Mkonda amewataka madereva wote nchini, hususan wale wanaoendesha magari ya masafa marefu ya kwenda mikoani, kuongeza umakini katika kipindi hiki ambacho mvua za masika zinaendelea kunyesha mikoa mbalimbali kusababisha uharibifu wa miundombinu.

Pia, amesema wanaendelea kuimarisha doria nchini kote ikiwemo kuzuia madereva wanaokatisha ruti huku akisema wataendelea kuwachukulia hatua kali za kisheria madereva wanaokiuka sheria na kanuni wakiwemo waendesha pikipiki, bajaji wasio na leseni.

Akizungumza Dar es Salaam,  Mkonda amesema, katika kipindi hiki cha mvua za masika wameendelea kuimarisha doria barabarani kote kushirikiana na Mamlaka zingine ikiwemo Mamlaka ya Udhibiti Barabarani (LATRA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADs), kuhakikisha zinapitika wakati wote", amesema.

“Katika kipindi hiki cha mvua za masika tumeendelea kuimarisha doria barabarani kote, kuhakikisha zinapitika pasi na shaka, wananchi waendelee na safari zao zenye lengo la kujenga uchumi wao na taifa", amesema.

“Katika kipindi hiki madereva waongeze umakini mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao, wachukue tahadhari wao kwa wao, waache mapuuza wanapokutana na maji yanapita juu ya daraja wasiwe na haraka wasubiri yapungue, kuepuka mwendokasi na kupita magari mengine bila tahadhari, kwani dereva makini ni yule anayejali mwenzake,”amesema

Aidha, amesema wanaendelea kuimarisha doria kote nchini kuhakikisha madereva, wote ikiwemo waendesha pikipiki, bajaji wanafuata na kuwa leseni, kanuni na alama za barabarani kuwachukulia hatua wote wanaokiuka, huku akiwatadharisha wale wanaokatisha ruti hususan mabasi ya ruti za mjini.