Na MWANDISHI WETU
Wanafunzi watatu wamefariki dunia baada kupigwa radi na wengine wawili kujeruhiwa.
Taarifa kwa umma iliyotolewa na Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam, imeeleza kuwa ajali hiyo ilitokea saa tano asubuhi, Msongola wilayani Ilala na kusababisha vigo vitatu na majeruhi wawili wote ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Msongola.
Waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni Alexander Paul, darasa la tano, Ally Pongwe darasa la tatu na Hudhaifa Shafi darasa la tano.
Waliojeruhiwa ni Nadri Maneno miaka darasa la tatu na Mahadi Ramadhan darasa la pili
ambao walipelekwa haraka hospitali ya karibu kwa matibabu.
Wakati huo huo, Polisi Dar es Salaam inachunguza tukio la mauaji ya
Athumani Nyanza, aliyegundulika kuuawa na kufukiwa kwenye shimo
pembeni ya nyumba yake Mtaa wa Kimya kimya, Zingiziwa, llala Dar es Salaam.
Polisi inatoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa zinazohusiana na usalama ili vitendo vya kihalifu viweze kuzuiwa.
