Vikundi zaidi ya 100 kupata mafunzo ya uchumi na ubunifu Dar
Na MWANDISHI WETU
ZAIDI ya vikundi 100 vya wajasiriamali wanawake kutoka Mkoa wa Dar es salaam, vinatarajia kupata mafunzo ya uwezeshaaji kiuchumi, kuongeza uelewa na ubunifu.
Hayo yamesemwa
na Mbunge wa Viti Maalumu , Amina Good Said,
ambaye ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Amo Foundation, jana.
Amina amesema mafunzo hayo yatafanyika Februari
13 mwaka huu, wilayani Ilala jijini Dar es Salaam.
“Tutayafanya
katika Ukumbi wa Blessing uliopo katika Kata ya Segerea. Vikundi zaidi ya 100 vitapata mafunzo
hayo bila malipo,”amesema.
Amina ameeleza
mafunzo hayo yatafunguliwa na Mjumbe wa
Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Halima Mamuya.
“Ni mafunzo
muhimu yatakayo walenga wanawake na makundi yote ya kinamama yanayofanya
shughuli za kiuchumi. Tunataka kuwajengea uelewa katika masuala mbalimbali ya kiuchumi na ubunifu wa shughuli zao,”amesema Amina.
Amebainisha dhamira
ni kuwasaidia wanawake hao kujiongezea kipato na masoko
ya uhakika ya bidhaa zao.
Reviewed by Gude Media
on
4:36:00 AM
Rating:


No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.