Kamati ya Miundombinu yataka atua zichukuliwe kwa wanaochezea mifumo ua udhibiti
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeiagiza Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), kuwachukua hatua kali za kisheria baadhi ya madereva wa mabasi hususan yale ya masafa marefu wanaochezea mifumo ya ufuatiliaji na udhibiti mwendo ijulikanayo kama VTS.
Hayo yamesemwa, jijini Dar es Salaam na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhandisi Jonhson Lutasingwa, ambaye ni Mbunge wa Bukoba Mjini, ameipongeza kamati hiyo kufanya ziara Ofisi za LATRA Dar es Salaam, huku wakiipongeza LATRA kwa kazi nzuri ya kuimarisha mifumo ya udhibiti wa vyombo hivyo vya usafirishaji abiria kupunguza ajali .
“Tunaipongeza serikali kupitia LATRA kwa kazi nzuri ambayo wanaifanya ya udhibiti ajali kwa njia ya mifumo. Tumejionea kazi kubwa inayofanywa hasa uimarishaji wa mifumo ya udhibiti mwendokasi , ambayo ni muhimu sana katika kuimarisha usalama.
“Kamati imeiagiza LATRA, kuendelea kuimarisha udhibiti huo, wawachukulie hatua wale wote wanaochezea mifumo, ambao siyo waaminifu katika mifumo hiyo wafuatilie na kuwachukuliwa hatua kali za kisheria,”amesema.
Ameeleza kuwa, agizo lingine walilotoa kwa LATRA nikuhakikisha wanashirikiana na vyombo vyingine vya udhibiti na usalama barabarani kuwezesha barabara hizo kupitika kwa wepesi na wananchi kupata huduma njema ya usafiri kuondoa mkanganyiko wa wawekezaji katika usafirishaji.
Reviewed by Gude Media
on
8:11:00 AM
Rating:



No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.