Bima ya Afya kwa wote yalenga makundi maalumu ya kimkakati
Na WAF, Dar es Salaam
Waziri wa Afya, Mohamed Mchengerwa amesema mpango wa Bima ya Afya kwa Wote umejikita kuyafikia makundi maalum ya kimkakati ikiwemo wafugaji, wakulima, wasanii, waendesha bodaboda na wachimbaji wadogo.
Mchengerwa ameyasema hayo leo Februari 2, 2026, wakati akizungumza katika kikao kazi na wahariri wa vyombo vya habari kilichofanyika Ukumbi wa Karimjee, Dar es Salaam.
Amesema dhamira kuu ya Serikali ni kumfuata mwananchi popote alipo kwa kutumia lugha na njia zinazoeleweka kwa kundi husika, ili kuongeza uelewa kuhusu Bima ya Afya kwa Wote na kuhamasisha usajili wa wananchi wengi zaidi.
Pia Mchengerwa amesema mpango huo pia utazingatia makundi yasiyo na uwezo, yakiwemo wazee, wajawazito na watu wenye ulemavu, ambao wataendelea kupatiwa huduma za matibabu bila malipo kwa mujibu wa utaratibu wa Serikali.
Aidha, ameeleza kuwa katika kuhakikisha taarifa za Bima ya Afya kwa Wote zinamfikia kila mwananchi, Serikali itaingiza ajenda ya bima katika shughuli za kila siku za kijamii na kiuchumi, pamoja na kutumia sanaa, wasanii na teknolojia ya habari katika kampeni za uhamasishaji.
Reviewed by Gude Media
on
12:07:00 PM
Rating:


No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.