Halmashauri Igunga yawazawadia wataalamu kwa kusimamia vizuri fedha za miradi ya maendeleo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Shabani Hemed, kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Selwa Hamid wametoa zawadi ya fedha sh. 400,000 na vyeti kwa wataalamu waliosimamia vema fedha zilizoletwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan.
Viongozi hao wametoa zawadi na pongezi hizo wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo mjini Igunga.
"Hakika sisi tunampongeza Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kuiletea Igunga fedha nyingi kutekeleza miradi ya maendeleo, hivyo tunawapongeza na kuwashika mkono watumishi hawa waliosimamia vema miradi yetu," amesema.
Aidha, wamegawa vyeti vya pongezi kwa Mkuu wa shule ya sekondari Mwisi, Baraka Magoma na Mganga Mfawidhi kituo cha afya Ziba, Kassim Hashim huku Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari, Seleka Mtobi na Mkuu wa Idara ya Idara ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Lucia Kafumu wakipongezwa kwa kuwasimamia kikamilifu watumishi hao.
Reviewed by Gude Media
on
6:01:00 AM
Rating:





No comments
Note: Only a member of this blog may post a comment.