Adha ya Mfereji yampa maradhi mwaka mmoja hajanyanyuka kitandani


Na MWANDISHI WETU

BALOZI wa Shina  Namba 8 la Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Kiburugwa  Salumu Abdallah, yuko hoi kitandani kwa mwaka mmoja sasa baada ya nyumba yake  kusombwa na mafuriko ya Mfereji wa   Shego, ulipo katika  kata hiyo wilayani Temeke, mkoani Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa  Jumuiya ya Wazazi  Wilaya ya Temeke, Hamis Slim, akiongozana na Diwani wa kata hiyo, Rashid  Chaburuma  pamoja naq viongozi wa Chama, walifika nyumbani kwa Salumu kumjulia hali ambapo ameeleza bado anasumbuliwa na maradhi tangu nyumba yake  iliposombwa na maji  na kuomba  jitihada  za kutatua kero hiyo  zifanyike.

Slim, alimhakikishia balozi huyo  kuwa dhamira kubwa ya kufika katika eneo hilo la Mfereji wa Shego ni baada ya kupokea malalamiko mengi  ya wanachama wa CCM, jumuia ya wazazi na wananchi kuhusu adha wanayoipata hasa kipindi cha mvua kutokana na mfereji huo kwa miaka mingi sasa.

“Tumefika hapa kukupa pole kwa sababu ulikuwa mstari wa mbele kueleza  kuhusu  changamoto ya mfereji huu. Chanzo cha maradhi  yako ni baada ya kupata adha ya mafuriko na miongoni mwa nyumba zilizo sombwa ni nyumba yako. Tunakupa pole na tutaendelea kupambana kuhakikisha  serikali yetu sikivu tunaishauri  kumalizia  sehemu ya  iliyobaki ya ujenzi wa mradi huo,”amesema Slimu.

Ameeleza awali  mfereji huo ulianza kutengenezwa katika Kata ya Charambe na kuishia katika Kata ya Kiburugwa lakini  haukumaliziwa hadi Kata ya Mbagala ambapo unaishia Mto Mzinga.

Slimu amesema mvua kubwa iliyoinyesha mwaka jana na mwaka juzi ilisababisha mafuriko yaliyoondoka na nyumba nyingi  za wakati wa eneo hilo.

“Ninaamini serikali ya CCM< chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, ipo katika utaratibu wa kuboresha mazingira hususan  miundombinu. Wananchi wawe watulivu kwa sababu  Rais  anaendelea kutekeleza kwa vitendo  ahadi yake  aliyoitoa ndani ya siku 100,”amesema Slim.

Kwa upande wa Diwani  wa Kata ya Kiburugwa, Rashid Chabruma, amesema  serikali imejipanga   kuendeleza ujenzi  na ujenzi wa mfereji huo hadi  kwa Manganya   ambapo jitihada kubwa zimekuwa zikifanywa na  Mbunge wa Mbagala  Bruchad Kakulu .

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kingugi, Kata ya Kiburugwa,  Athumani  Magenge,  ameeleza  Mfereji wa Shego umekuwa adha kubwa kwa wananchi wa Mitaa ya Kingugi, Kwa nyoka na Magenge.

“Eneo hili limeaghiri zaidi ya kaya 300. Wengi walihifadhiwa katika ofisi zetu kwa zaidi ya miezi mitatu baada ya mvua kubwa kunyesha mwaka jana na mwaka juzi. Zimebaki kilometa tano tu kumalizia ujenzi wa  mfereji huyo. Mfereji huu unaendelea kutanuka na kuathiriwa,”amesema.

 Ameiomba serikali kuwafikiria wananchi wa Kiburugwa kujenga mfereji huo  ili kunusuru  wananchi  na kuondokana na adha kubwa wanayoipata mvua inapo nyesha. 



Adha ya Mfereji yampa maradhi mwaka mmoja hajanyanyuka kitandani Adha ya Mfereji  yampa maradhi  mwaka mmoja hajanyanyuka kitandani Reviewed by Gude Media on 10:46:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.