Shilingi bilioni 11.3 kuzalisha vitambulisho vya watoto

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene (kulia) akioneshwa ukaguzi wa kitambulisho kwa kutumia mfumo uliowekwa kwenye simu na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Omar Mmanga. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).



Na Mwandishi Wetu


Serikali iko katika  maandalizi ya usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka 18, kutoa namba ya utambulisho ya kipekee ambayo itakayotolewa tangu mtu anapozaliwa hadi mwisho wa maisha yake ikiwa ni Utekelezaji wa Maelekezo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, aliyotoa Agosti 10, 2023.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene wakati wa ziara ya ukaguzi wa uzalishaji wa vitambulisho katika Kituo cha Kuchakata Taarifa  cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa(NIDA).


Simbachawene alisema Shilingi Bilioni 11.3 kutengwa kwa ajili ya mpango huo, ambapo  wilaya za majaribio zikiwa ni Kilolo, Kusini Unguja na Rungwe.


"Jamii namba itakayotambua watoto ndio jambo kubwa ambalo linakuja sasa na itaondoa malalamiko mbalimbali kwani mtu atakua anatambulika kuanzia pale anapozaliwa, pia nawasihi watanzania ama ni walowezi ama wakimbizi na wengine wakawa wameombea kazi utambulisho sio wao au walisomea majina sio yao wakaondolewa kazini umetolewa msamaha na  Rais Dk. Samia, waje wasafishe taarifa zao za utambuzi warudi kwenye majina yao yanayotambulika kwa kuwa hayo waliyokua wameyatumia yataendelea kuwaletea matatizo wakati wote", amesema.


"Wengine wameondolewa kazini kwa vyeti feki na wengine wameshindwa kupata uraia kwa kuwa walitoa taarifa ambazo sio sahihi na wengine waliomba vitambulisho zaidi ya mara moja",  amesema Waziri Simbachawene.


Simbachawene ameongeza pia kuna vitambulisho ambavyo vimezalishwa na wahusika hawajafika kuchukua akiwataka kufika vituo mbalimbali katika wilaya walizojiandikishia ili kuchukua vitambulisho vyao huku akiweka wazi ukomo wa matumizi ya namba ya utambulisho (NIN) kuwa ni miaka mitatu.


‘Watu wafike katika maeneo waliyojiandikisha kuchukua vitambulisho vyao kwani kitambulisho cha NIDA hivi sasa kimeunganishwa na Kadi ya Bima ya Afya, leseni ya udereva na mifuko ya hifadhi ya jamii hatua ambayo imemrahisishia mwananchi pindi anapotaka kupata huduma za kiafya au mfuko wa jamii", amesema.


Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu  wa Mamlala ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Omar Mmanga, amesema mamlaka inaendelea na utambuzi na usajili  wa watanzania wanaoishi nje ya nchi (diaspora) ambapo jumla ya watanzania 1465  wanaoishi nje ya nchi wametambuliwa na kuandikishwa mpaka sasa huku lengo ikiwa kuwafikia watanzania wote wawe na utambulisho popote walipo ambapo mpaka sasa jumla ya vitambulisho 21,245,975 vikiwa vimezalishwa nchini.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akikagua vitambulisho vilivyozalishwa wakati wa ziara ya ukaguzi wa vitambulisho hivyo uliofanyika katika Kituo cha Kuchakata Taarifa cha Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA). Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Omar Mmanga na kulia ni Meneja Uzalishaji Vitambulisho vya Taifa, Jeremia Kiverege. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).



Shilingi bilioni 11.3 kuzalisha vitambulisho vya watoto Shilingi bilioni 11.3 kuzalisha vitambulisho vya watoto Reviewed by Gude Media on 12:24:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.