UVCCM Igunga yamuombea kura za kishindo Dk. Samia


IGUNGA - TABORA 

KATIBU wa  Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, Gamalu Makona  ameendelea kumuombea kura za kishindo Mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Samia Suluhu Hassan.


Gamalu ameendelea na zoezi hilo wakati alipokua na Kamati ya utekelezaji ya UVCCM Wilaya kuhamasisha makundi maaulumu ya  Bodaboda, Mamalishe, Mafundi Seremala, Mawakala wa Mabasi katika kata ya Chabutwa, Ziba na Ibologero wilayani Igunga.


Aidha, ametoa elimu kwa makundi hayo namna sahihi ya kupiga kura kwa kutumia 

karatasi ya mfano wa kupigia kura kwa lengo la kuhakikisha kura zitakazo pigwa haziaribiki na watie tiki au alama ya vema katika kisanduku cha mgombea wa chama hicho.


"Nawaelekeza wananchi wetu namna sahihi ya kupiga kura ndani ya kisanduku au kiboksi na niwaombe mfikishe elimu hii kwa  wale waliyoko majumbani," ameomba Gamalu.






UVCCM Igunga yamuombea kura za kishindo Dk. Samia UVCCM Igunga yamuombea kura za kishindo Dk. Samia Reviewed by Gude Media on 12:32:00 PM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.