Wasimamizi wasaidizi ngazi kata wapewa mafunzo

 

IGUNGA - TABORA 

MSIMAMIZI wa Uchaguzi  Jimbo la Igunga na Manonga mkoani Tabora, Hamisi Hamisi ameendelea kukagua mafunzo ya kuwajengea  uwezo Wasimamizi Wasaidizi ngazi ya kata kwa lengo la kuhakikisha watasimamia vema taratibu za uchaguzi mkuu katika maeneo yao.

Hamisi amefanya ukaguzi huo wakati mafunzo hayo ya Uchaguzi ambayo  yanaingia siku ya pili yanayofanyika  kwa wasimamizi hao katika ukumbi wa Maxwel mjini hapa.


Aidha, amewataka Wasimamizi hao kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na maelekezo yanayotolewa na Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi muda wote wa utendaji wa majukumu yao.


Amesema hatua hiyo itaweupesha   na  makosa ya kila aina wakati wa zoezi hilo, hivyo watahakikisha uchaguzi unafanyika kwa ufanisi, amani na utulivu chini ya kauli mbiu isemayo:" Kura Yako Haki Yako, Jitokeze Kupiga Kura".




Wasimamizi wasaidizi ngazi kata wapewa mafunzo Wasimamizi wasaidizi ngazi kata wapewa mafunzo Reviewed by Gude Media on 1:51:00 AM Rating: 5

No comments

Note: Only a member of this blog may post a comment.